Mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania anaishi Sweden Rachel
Sharp siku ya Jumamosi aliongea na waandishi wa habari na blogger nyumbani
kwake Tegeta kuhusiana na ujio wake mpya wa albamu yake ya pili ya “NI MUNGU WA
AJABU” ambayo iko katika mfumo wa audio na video.
Mwimbaji huyu kwa sasa anaishi nchini Sweden na ambako
anafanaya huduma ya kumtangaza Kristo na ni majasiliamali.
Rachel Sharp
Rachel Sharp
Rachel Sharp aliwahimiza watu kupenda utamaduni wao na
kuachana na tabia ya kukopi tamaduni za watu. Alisisitiza sana kuwa kama
Watanzania tunatakiwa kuwa na mfumo wetu wa uimbaji ambao utafanya watu wengine
kuupenda kutamani kufanya kama sisi. Alisema “Watu wamekuwa wakipenda sana
nyimbo za Afrika Kusini kuliko nyimbo za wazawa..tunatakiwa kubadilika”
Rachel Sharp alimshukuru sana Mungu wa hatua aliyofikia ya
uimbaji kwani, alikotokani mbali sana.
Rachel kwa sasa ni mama mwenye watoto wawili wanaoishi nchini Sweden na ni mama aliolewa na mzungu wa Kiswedeni. Hivi sasa yuko nchini Tanzania kwa likizo fupi, na baada ya hapo atarudi nchini Sweden kwa majukumu mengine
Press release
Rachel kwa sasa ni mama mwenye watoto wawili wanaoishi nchini Sweden na ni mama aliolewa na mzungu wa Kiswedeni. Hivi sasa yuko nchini Tanzania kwa likizo fupi, na baada ya hapo atarudi nchini Sweden kwa majukumu mengine
Press release
KARIBUNI sana
wanahabari katika hafla yetu hii fupi
yenye lengo la kumpa Mungu wetu utukufu. Mimi ninaitwa Rachel Scharp, ni
Mwimbaji wa nyimbo za Injili, ninaishi Malmo Sweden. Lakini kwa sasa nipo
nyumbani kwa ajili ya utambulisho wa Albamu yangu ya Mziki wa Injili.
Uimbaji kwangu ni
maisha kwa kuwa nilianza kuupenda muziki na kuimba nikiwa mdogo sana, nilikuwa
nikitunga nyimbo na kuwafundisha wadogo zangu. Tuliimba nyimbo hizo jioni, haswa kwa kipindi kile cha
ugawaji ikiwa zamu ya kwaya yetu, ile foleni ya kununua mchele iliyokuwa ndefu
chakula kilikuwa kinachelewa, ili wadogo zangu wasilale bila kula na furaha ya
kusubiria ubwabwa na maharage basi tunaimba kusubiria msosi. Wakati huo
hakukuwa na TV kama ilivyo sasa.
Niliimba kwaya ya shule pale “Jangwani Secondary” pia
niliongoza sifa na kuabudu kwenye Fellowship katika Kanisa la Msewe Lutheran.
Nilikuwa nikiandika nyimbo nyingi nikitegemea kupata fursa ya kurekodi na
kuimba na Kwaya nyimbo zangu, lakini sikupata fursa hiyo.
Kwa sasa ninaimba
kwaya ya Kanisa la Elim Pentecostal huko Malmo Kusini mwa Sweden, ninaongoza
sifa na kuabudu. Ninaimba pia kwenye kundi linaloitwa Shalom International
ambalo ni muunganiko wa waimbaji kutoka makanisa mbali mbali ya Kiroho yaliyopo
mjini Malmo. Nilipata fursa ya kurekodi albam yangu ya kwanza mwaka 2008
nikazinduliwa huko Sweden, Mei mwaka 2009 nikisindikizwa na dada Upendo
Kilahiro. Albam hiyo niliita ‘Nalinga na Yesu’ yenye nyimbo 9, iko kwenye mfumo
wa sauti tu.
Leo ninatambulisha
album yangu ya Pili yenye jina la ‘Ni Mungu wa Ajabu’. Album hii ina nyimbo
kumi zilizo kwenye mfumo wa sauti (audio), na 8 kwenye mfumo wa Picha na Sauti
(DVD). Nimerekodi album hii Oktoba mwaka 2011 nchini Sweden, kwa upande wa
mpangilio wa vyombo na muziki nikisaidiwa na Paalab Nyarko, kutoka Ghana na
Producer Zillile Matikinga (Zorro) – kutoka South Afrika.
Mwanzoni mwa mwaka 2012 niliongeza na baadhi ya vionjo
vya muziki kwenye studio za New Life Band Arusha, vionjo nilivyoingiza ni gitaa
la solo lililopigwa na Godlucky Matingisa wa New Life Band Arusha, Base gitaa
limepigwa na Wilson Godfrey Mtangoo. Ngoma zilipigwa na Fujo Makaranga. Na
sauti pia niliingiza hapo Arusha nikisaidiwa na Jackson Benty, chini ya
usimamizi na uangalizi wa Producer Wilson Mtangoo. Mwalimu wa sauti ni
Mchungaji David Nkone.
Video imerekodiwa na UMU Production Arusha chini ya
uongozi wa Jojo Jose Mwakajila. Video hii imerekodiwa Sweden (Malmo), Ujerumani
(Berlin), Tanzania (Dar es Salaam, Bagamoyo, Arusha, Moshi, Serengeti).
Midundo ya nyimbo ni
ya kiasili (kitamaduni). Napenda nyimbo zenye vionjo vya Kiafrika na Kitanzania
zaidi. Nimeimba kwa Kiswahili na Kiingereza pia. Na nyimbo nyingi ni za
Kiswahili, hii haimanishi kwamba soko liko nchi wanazoongea Kiswahili tu. Cha
kushangaza ni kwamba pia nchi za Scandinavia wanapenda san Kiswahili na
kukithamini, na nafikiri kuliko hata sisi wenye lugha.
Wanasema kwamba ni
lugha yenye sauti tamu name sina budi kujivunia na kuiendeleza na huku
nikimsifu Mungu na kupeleka ujumbe kwa watu wake.
Nyimbo hizi zimebeba
ujumbe mbali mbali, kuna za kumsifu Mungu na matendo yake makuu, kuna za maonyo
na kuna za kutia moyo kwa safari hii ngumu ya kwenda Mbinguni.
Ningependa sana watu wapate ujumbe huu na wakutane na
Mungu katika maeneo hayo tofauti kama nilivyoeleza mwanzoni kuwa kuna kumsifu
na kumwabudu Mungu, kuonywa na kutiwa moyo pia. Inategemea mtu yuko kwenye hali
gani na ana mahitaji gani.
WITO WANGU KWA JAMII
Kwanza ni kupenda na
kuthamini kile tulicho nacho Mungu alichotupatia. Kwanza kwa sisi wakristo
tumepewa Neema hii ya wokovu tunatakiwa tuipende, tuithamini, tuitunze na
tuiendeleze, tusiichezee na tuwafanye wengine pia waijue na waipate.
Kama tusipoipenda,
tusipoithamini, kujivunia na kuilinda, wengine hawatajua thamani yake.
Nikija kwenye jamii yetu kwa sasa tunapenda sana kuiga kutoka nje tunaacha ya kwetu, sikatai
kuiga yale yaletayo maendeleo, na tunahitaji kujifunza kutoka kwa walioendelea,
lakini si kwamba tuvipuuzie vya kwetu. Kuna vyetu vinavyohitaji mwendelezo. Na
tene vikawa vizuri sana na wan je wakaiga kutoka kwetu. Kwa mfano; muziki wetu,
lugha yetu na vingine vingi.
Kwa upande wa muziki, Watanzania siku hizi wanapenda
sana muziki kutoka Afrika Kusin, ni mzuri sana hata mimi ninapendezwa nao.
Naona sasa waimbaji wengi wanapenda kuiga mtindo huo. Ule ni muziki wa asili wa
ngoma zao za kienyeji ukawekewa/ukaongezewa vionjo vya kisasa.
Sasa na sisi
tutakapopiga mziki huo hautakuwa mzuri kama wanavyopiga Joyous Celebration kwa
kuwa ndio asili yao. Swali ni kwamba, kwa nini sisi Watanzania tusitengeneze
lizombe letu au Mdumange au Sindimba na hata Mdundiko tukaweka vionjo vya
kisasa ukawa mzuri na wao waige kutoka kwetu? Nilazima tujitahidi jamani tuwe
na utambulisho wetu (identity).
Kwamba ukisikika muziki uutambue mmmh Huu ni muziki wa Tanzania, tunahitaji
ubunifu tu kuondoa uvivu wa kufikiri. Kama tukitulia na kubuni na kutumia
vipawa tulivyopewa na Mungu tutafika mbali sana na sio kupita njia ya mkato ya
kuiga tu.
Ninamaliza kwa
kuwaambia Watanzania, tusiende kwa mazoea eti watu wamezoea hivi. Huu ni wakati
wa mabadiliko, tubadilike turudi kwetu. Tutafika mbali. Watanzania tunaweza, na
kuleta mabadilikoni mimi na wewe.
Rachel akicheza sawa na Bloggers Uncle Jimmy na Rulea Sanga.
MC na mtangazaji wa Wapo Radio, Ritha Chiwalo akifanya utambulisho.
Bloga Papa (kushoto) akiwa makini katika kazi ya urushaji habari
mitandaoni, anayefuatia ni mwimbaji wa nyimbo za injili Tanzania, Upendo
Kilahiro akiwa na mwanae.
Master Prophet Machibya akitambulishwa na MC Ritha Chiwalo
MC Chiwalo akimsikiliza mtoto wa Upendo Kilahiro akijitambulisha akiwa na mtoto wake Ritha Chiwalo
Baadhi ya wageni na waandishi wa habari wakiwa nyumbani kwa Rachel Sharp wakiomba
Walioko mbele ni mama wa Rachel Sharp (kulia) akiwa na mwanae Rachel Sharp wakati wa utambulisho
Rachel Sharp akisoma Press Release kwa waandishi wa habari na bloggers
Master Prophet Machibya akipokea mic kutoka kwa MC Ritha kwaajili ya kuanza zoezi la kuombea albamu ya Rachel Sharp
Mtangazaji wa Clouds na blogger Samsasali akifanya mahojiano na Upendo Kilahiro
Rachel Sharp akimchezea Mungu wetu kwa furaha
Master Prophet Machibya akifanaya mahojiano kuhusiana na ujio mpya wa Rachel Sharp
Master Prophet Machibya wakiwa na Rachel Sharp katika picha ya pamoja baada ya kuiombea albamu
Bloggers Rulea Sanga (kulia) na Samsasali wakicheki matukio
Wakati wa msosi
Mtangazaji wa radio, Erick Brighton (kulia)
Mchekeshaji Chavala akiwa katika mawasiliano
Rachel Sharp akiwapongeza watu waliofika kwa makofi
Baadhi ya waandishi wa habari wakimchukua mwimbaji wa nyimbo za injili Tanzania, Upendo Kilahiro wakati akaiimba.
Rachel akitambulisha wazazi wake
Rachel Sharp na Nabii Machibya wakati wa kuombea albamu mpya
Chavala akiwavunja mbavu waliofika katika hafla hii.
Ma Bloggers Kulia Kutoka Shalom na kushoto Kutoka Rejoice ndani ya eneo la tukio
Upendo Kilahiro na Rachel Sharp
Ze Blogger Samsasali na Kilahiro
Upendo Kilahiro akiwa anafanya performance siku ya leo nyumbani kwa Rachel
---------------------------------------------------
PICHA NA HABARI ZIMEANDALIWA NA
---------------------------------------------------
PICHA NA HABARI ZIMEANDALIWA NA
Rulea Sanga
Creative Director and Graphic Designer
RUMAFRICA
Mob: +255 715851523
Email: rumatz2012@gmail.com