FANUEL SEDEKIA - "JINA LA YESU" SONG

Thursday, January 31, 2013

RACHEL SHARP AWAKUTANISHA WAANDISHI WA HABARI NA BLOGGERS KUTAMBULISHA ALBAMU YAKE NA KUZUNGUMZIA UMUHIMU WA KUTUMIA NYIMBO ZA ASILI ZA INJILI KUFIKISHA UJUMBE WA MUNGU KWA WATU WOTE


Mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania anaishi Sweden Rachel Sharp siku ya Jumamosi aliongea na waandishi wa habari na blogger nyumbani kwake Tegeta kuhusiana na ujio wake mpya wa albamu yake ya pili ya “NI MUNGU WA AJABU” ambayo iko katika mfumo wa audio na video.
Mwimbaji huyu kwa sasa anaishi nchini Sweden na ambako anafanaya huduma ya kumtangaza Kristo na ni majasiliamali.
Rachel Sharp
Rachel Sharp aliwahimiza watu kupenda utamaduni wao na kuachana na tabia ya kukopi tamaduni za watu. Alisisitiza sana kuwa kama Watanzania tunatakiwa kuwa na mfumo wetu wa uimbaji ambao utafanya watu wengine kuupenda kutamani kufanya kama sisi. Alisema “Watu wamekuwa wakipenda sana nyimbo za Afrika Kusini kuliko nyimbo za wazawa..tunatakiwa kubadilika”

Rachel Sharp alimshukuru sana Mungu wa hatua aliyofikia ya uimbaji kwani, alikotokani mbali sana.

Rachel kwa sasa ni mama mwenye watoto wawili wanaoishi nchini Sweden na ni mama aliolewa na mzungu wa Kiswedeni. Hivi sasa yuko nchini Tanzania kwa likizo fupi, na baada ya hapo atarudi nchini Sweden kwa majukumu mengine


Press release
KARIBUNI sana wanahabari katika hafla yetu hii fupi  yenye lengo la kumpa Mungu wetu utukufu. Mimi ninaitwa Rachel Scharp, ni Mwimbaji wa nyimbo za Injili, ninaishi Malmo Sweden. Lakini kwa sasa nipo nyumbani kwa ajili ya utambulisho wa Albamu yangu ya Mziki wa Injili.
Uimbaji kwangu ni maisha kwa kuwa nilianza kuupenda muziki na kuimba nikiwa mdogo sana, nilikuwa nikitunga nyimbo na kuwafundisha wadogo zangu. Tuliimba nyimbo  hizo jioni, haswa kwa kipindi kile cha ugawaji ikiwa zamu ya kwaya yetu, ile foleni ya kununua mchele iliyokuwa ndefu chakula kilikuwa kinachelewa, ili wadogo zangu wasilale bila kula na furaha ya kusubiria ubwabwa na maharage basi tunaimba kusubiria msosi. Wakati huo hakukuwa na TV kama ilivyo sasa.
Niliimba kwaya ya shule pale “Jangwani Secondary” pia niliongoza sifa na kuabudu kwenye Fellowship katika Kanisa la Msewe Lutheran. Nilikuwa nikiandika nyimbo nyingi nikitegemea kupata fursa ya kurekodi na kuimba na Kwaya nyimbo zangu, lakini sikupata fursa hiyo.
Kwa sasa ninaimba kwaya ya Kanisa la Elim Pentecostal huko Malmo Kusini mwa Sweden, ninaongoza sifa na kuabudu. Ninaimba pia kwenye kundi linaloitwa Shalom International ambalo ni muunganiko wa waimbaji kutoka makanisa mbali mbali ya Kiroho yaliyopo mjini Malmo. Nilipata fursa ya kurekodi albam yangu ya kwanza mwaka 2008 nikazinduliwa huko Sweden, Mei mwaka 2009 nikisindikizwa na dada Upendo Kilahiro. Albam hiyo niliita ‘Nalinga na Yesu’ yenye nyimbo 9, iko kwenye mfumo wa sauti tu.
Leo ninatambulisha album yangu ya Pili yenye jina la ‘Ni Mungu wa Ajabu’. Album hii ina nyimbo kumi zilizo kwenye mfumo wa sauti (audio), na 8 kwenye mfumo wa Picha na Sauti (DVD). Nimerekodi album hii Oktoba mwaka 2011 nchini Sweden, kwa upande wa mpangilio wa vyombo na muziki nikisaidiwa na Paalab Nyarko, kutoka Ghana na Producer Zillile Matikinga (Zorro) – kutoka South Afrika.
Mwanzoni mwa mwaka 2012 niliongeza na baadhi ya vionjo vya muziki kwenye studio za New Life Band Arusha, vionjo nilivyoingiza ni gitaa la solo lililopigwa na Godlucky Matingisa wa New Life Band Arusha, Base gitaa limepigwa na Wilson Godfrey Mtangoo. Ngoma zilipigwa na Fujo Makaranga. Na sauti pia niliingiza hapo Arusha nikisaidiwa na Jackson Benty, chini ya usimamizi na uangalizi wa Producer Wilson Mtangoo. Mwalimu wa sauti ni Mchungaji David Nkone.
Video imerekodiwa na UMU Production Arusha chini ya uongozi wa Jojo Jose Mwakajila. Video hii imerekodiwa Sweden (Malmo), Ujerumani (Berlin), Tanzania (Dar es Salaam, Bagamoyo, Arusha, Moshi, Serengeti).
Midundo ya nyimbo ni ya kiasili (kitamaduni). Napenda nyimbo zenye vionjo vya Kiafrika na Kitanzania zaidi. Nimeimba kwa Kiswahili na Kiingereza pia. Na nyimbo nyingi ni za Kiswahili, hii haimanishi kwamba soko liko nchi wanazoongea Kiswahili tu. Cha kushangaza ni kwamba pia nchi za Scandinavia wanapenda san Kiswahili na kukithamini, na nafikiri kuliko hata sisi wenye lugha.
Wanasema kwamba ni lugha yenye sauti tamu name sina budi kujivunia na kuiendeleza na huku nikimsifu Mungu na kupeleka ujumbe kwa watu wake.
Nyimbo hizi zimebeba ujumbe mbali mbali, kuna za kumsifu Mungu na matendo yake makuu, kuna za maonyo na kuna za kutia moyo kwa safari hii ngumu ya kwenda Mbinguni.
Ningependa sana watu wapate ujumbe huu na wakutane na Mungu katika maeneo hayo tofauti kama nilivyoeleza mwanzoni kuwa kuna kumsifu na kumwabudu Mungu, kuonywa na kutiwa moyo pia. Inategemea mtu yuko kwenye hali gani na ana mahitaji gani.
WITO WANGU KWA JAMII
Kwanza ni kupenda na kuthamini kile tulicho nacho Mungu alichotupatia. Kwanza kwa sisi wakristo tumepewa Neema hii ya wokovu tunatakiwa tuipende, tuithamini, tuitunze na tuiendeleze, tusiichezee na tuwafanye wengine pia waijue na waipate.
Kama tusipoipenda, tusipoithamini, kujivunia na kuilinda, wengine hawatajua thamani yake.
Nikija kwenye jamii yetu kwa sasa tunapenda sana  kuiga kutoka nje tunaacha ya kwetu, sikatai kuiga yale yaletayo maendeleo, na tunahitaji kujifunza kutoka kwa walioendelea, lakini si kwamba tuvipuuzie vya kwetu. Kuna vyetu vinavyohitaji mwendelezo. Na tene vikawa vizuri sana na wan je wakaiga kutoka kwetu. Kwa mfano; muziki wetu, lugha yetu na vingine vingi.
Kwa upande wa muziki, Watanzania siku hizi wanapenda sana muziki kutoka Afrika Kusin, ni mzuri sana hata mimi ninapendezwa nao. Naona sasa waimbaji wengi wanapenda kuiga mtindo huo. Ule ni muziki wa asili wa ngoma zao za kienyeji ukawekewa/ukaongezewa vionjo vya kisasa.
Sasa na sisi tutakapopiga mziki huo hautakuwa mzuri kama wanavyopiga Joyous Celebration kwa kuwa ndio asili yao. Swali ni kwamba, kwa nini sisi Watanzania tusitengeneze lizombe letu au Mdumange au Sindimba na hata Mdundiko tukaweka vionjo vya kisasa ukawa mzuri na wao waige kutoka kwetu? Nilazima tujitahidi jamani tuwe na utambulisho wetu (identity). Kwamba ukisikika muziki uutambue mmmh Huu ni muziki wa Tanzania, tunahitaji ubunifu tu kuondoa uvivu wa kufikiri. Kama tukitulia na kubuni na kutumia vipawa tulivyopewa na Mungu tutafika mbali sana na sio kupita njia ya mkato ya kuiga tu.
Ninamaliza kwa kuwaambia Watanzania, tusiende kwa mazoea eti watu wamezoea hivi. Huu ni wakati wa mabadiliko, tubadilike turudi kwetu. Tutafika mbali. Watanzania tunaweza, na kuleta mabadilikoni mimi na wewe.
Asanteni sana kwa kuja kushiriki pamoja name tukio hili la Baraka. Mungu awabariki sana.Rachel Scharp
 Rachel akicheza sawa na Bloggers Uncle Jimmy na Rulea Sanga.
 MC na mtangazaji wa Wapo Radio, Ritha Chiwalo akifanya utambulisho.
 Bloga Papa (kushoto) akiwa makini katika kazi ya urushaji habari mitandaoni, anayefuatia ni mwimbaji wa nyimbo za injili Tanzania, Upendo Kilahiro akiwa na mwanae.
 Master Prophet Machibya akitambulishwa na MC Ritha Chiwalo
 MC Chiwalo akimsikiliza mtoto wa Upendo Kilahiro akijitambulisha akiwa na mtoto wake Ritha Chiwalo
 Baadhi ya wageni na waandishi wa habari wakiwa nyumbani kwa Rachel Sharp wakiomba
 Walioko mbele ni mama wa Rachel Sharp (kulia) akiwa na mwanae Rachel Sharp wakati wa utambulisho
 Rachel Sharp akisoma Press Release kwa waandishi wa habari na bloggers
 Master Prophet Machibya akipokea mic kutoka kwa MC Ritha kwaajili ya kuanza zoezi la kuombea albamu ya Rachel Sharp
 Mtangazaji wa Clouds na blogger Samsasali akifanya mahojiano na Upendo Kilahiro
 Rachel Sharp akimchezea Mungu wetu kwa furaha
 Master Prophet Machibya akifanaya mahojiano kuhusiana na ujio mpya wa Rachel Sharp
 Master Prophet Machibya wakiwa na Rachel Sharp katika picha ya pamoja baada ya kuiombea albamu
 Bloggers Rulea Sanga (kulia) na Samsasali wakicheki matukio
 Wakati wa msosi



 Mtangazaji wa radio, Erick Brighton (kulia)

 Mchekeshaji Chavala akiwa katika mawasiliano

 Rachel Sharp akiwapongeza watu waliofika kwa makofi
 Baadhi ya waandishi wa habari wakimchukua mwimbaji wa nyimbo za injili Tanzania, Upendo Kilahiro wakati akaiimba.
 Rachel akitambulisha wazazi wake

 Rachel Sharp na Nabii Machibya wakati wa kuombea albamu mpya
 Chavala akiwavunja mbavu waliofika katika hafla hii.




Ma Bloggers Kulia Kutoka Shalom na kushoto Kutoka Rejoice ndani ya eneo la tukio

Upendo Kilahiro na Rachel Sharp
 Ze Blogger Samsasali na Kilahiro
 Upendo Kilahiro akiwa anafanya performance siku ya leo nyumbani kwa Rachel
---------------------------------------------------
PICHA NA HABARI ZIMEANDALIWA NA
Rulea Sanga
Creative Director and Graphic Designer
RUMAFRICA
Mob: +255 715851523
Email: rumatz2012@gmail.com

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...